Msanii wa kizazi Kipya Diamond Platinum Akiongea na Miss Jestina Goerge kuhusu show zake London na kuweka wazi uhusiano wake yeye na Wema Sepetu.
“NIMPENDE NANI”-DIAMOND (NEW SONG)
Jina la wimbo huu mpya kutoka kwa Diamond linaweza kukushtua kidogo hususani kama wewe ni mfuatiliaji wa habari za kwenye luninga,magazetini na bila shaka kwenye blogs na social networks zingine ambako mengi hujiri siku hizi! Ila kama hufuatilii basi ntakupa kiduchu…Diamond ni mpenzi wa Wema Sepetu.At least hivyo ndivyo inavyojulikana miongoni mwa wengi kupitia “live” screens za magazetini nk.Sasa wiki hii kumekuwepo na dodoso lukuki kwamba Diamond hayupo tena na Wema na kahamishia mahaba yake kwa Jokate Mwegelo,mlimbwende,mshehereshaji na pia fashion designer.Aliyetoa “siri” ni Wema Sepetu mwenyewe kupitia kipindi cha Zamaradi cha Take One pale Clouds TV.
Wakati yote hayo yanajiri,wimbo mpya wa Diamond unaingia sokoni.Unaitwa NIMPENDE NANI?Ni kutoka katika album aliyoiingiza sokoni hivi karibuni inayokwenda kwa jina Lala Salama. A coincidence? Kali zaidi ni maneno yaliyopo katika wimbo huu.In case unajiuliza ulitungwa lini,ninachoweza kukwambia ni kwamba ulitungwa muda mrefu.Sasa iweje uwe kama vile unaendana na matukio ya sasa,go figure out!Usikilize
Comments
Post a Comment