Wema afunguka kuhusu habari ya gazeti..mp3 - Hulk Share - Music Distribution Platform



W&K



















Baada ya Kanumba kufunguka kuhusiana na kuchukizwa kwa habari iliyotolewa kwenye gazeti kuhusiana na kurudisha mahosiano kwa Wema Sepetu, Wema naye amefunguka na kucheck kwenye simu na kuniambia amechoka na haya magazeti kuhusu yeye kila siku ili kuweka msisitozo akaamua kunitumia Voice Note ili mumsikie kabisa.

FROM;DJCHOKABLOGPOST

Wema afunguka kuhusu habari ya gazeti..mp3 - Hulk Share - Music Distribution Platform



Dalili 4 za mwanaume aliye tayari kwa maisha ya ndoa!



Mpenzi msomaji wangu, wiki hii nataka kuzungumzia kwa kifupi dalili nne za mwanaume aliye tayari kuingia katika maisha ya ndoa. Ni dalili za kitaalam na ukiona huyo uliye naye anazo, una kila sababu ya kumshawishi akuoe tena haraka sana lakini usipoziona ikiwezekana hata ndugu zako wasimjue kwani ni wazi hamuwezi kuingia kwenye maisha ya ndoa ya kueleweka.
Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaume wanaoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuoa kila siku ni wengi lakini je wanaoolewa wote wanaingia kwenye maisha ya ndoa na watu sahihi? Jibu ni hapana, na hii ni kwa sababu wanawake wengine wanakubali kuolewa na wanaume ambao hawakujiandaa kuingia kwenye maisha hayo. Dalili zenyewe ni hizi hapa chini.

Waliobaini kuwa ni muda mufaka
Unaweza kuwa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye umri wake umekwenda lakini bado anaona anastahili kuwa kwenye maisha ya ‘ubachela’. Ukikubali kuolewa na mwanaume wa sampuli hii lazima atakusumbua lakini yule ambaye amekaa, akatafakari kisha akagundua kuwa ni wakati muafaka wa kuoa, ni wazi huyo atakuwa amejiandaa na hata ukimkubalia sidhani kama utajuta.


Anajiamini, siyo tegemezi
Ni kweli mapenzi hayana uhusiano wowote na fedha lakini ukweli usiofichika ni kwamba kama mwanaume hana kazi inayomuwezesha kumuingizia kipato, hawezi kuwa miongoni mwa wale wanaostahili kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Ukikubali kuolewa na mwanaume asiye na kitu eti kwa sababu tu umempenda na moyo wako hauko tayari kumkosa, ujue unajiingiza kwenye maisha ya bahati nasibu kitu ambacho siyo kizuri. Kama huyo uliyenaye siyo tegemezi, ni mtu mwenye uwezo wa kukulisha na kukutimizia shida zako zinazohitaji fedha, usione hatari kumwambia afanye hima akatoe mahari muoane.

Anachukua nafasi ya baba
Kuna baadhi ya wanaume licha kwamba hawajaingia kwenye maisha ya ndoa na hawajafanikiwa kuwa na watoto lakini wameshaanza kuzishika nafasi za ‘ubaba’. Unaweza kuwa na mpenzi akawa ni mtu wa kupenda sana watoto na wakati mwingine kuzungumzia namna wa kwake watakavyokuwa. Huyu ni mwanaume ambaye ana dalili za kutaka kuingia kwenye maisha ya ndoa.


Anakuchukulia kama mke wake
Chukulia kwamba uko na mpenzi wako lakini jinsi anavyokuchukulia ni kama mke wake. Kwa kifupi utaanza kumuona anachukua nafasi ya mume. Kwa mfano ataanza kuweka mikakati kwa ajili ya maisha yenu ya baadae, atakutambulisha kwa ndugu, jamaa na marafiki zake, atakuwa akikushirikisha katika kila suala linalogusa maisha yako na yake.
Aidha, mtaalam wa masuala ya mapenzi nchini Marekani, Carol Morgan anaongeza kuwa, licha ya yote hayo pia mwanaume huyo atakuwa ni mkweli na muwazi katika kila jambo.
 Hizo ni dalili nne za mwanaume ambaye amejiandaa kuingia katika maisha ya ndoa.  Kwa leo niishie hapo, niwatakie kila la kheri katika mwaka mpya unaokuja.

vMwaka umekwisha, unakaribia  kustaafu, kuzeeka umejiandaaje?

Inawezekana ninaposema kustaafu wewe kama msomaji wangu unadhani kuwa, nawazungumzia wale walioajiriwa serikalini au kwenye mashirika peke yao. La hasha! Maana yangu kubwa hapa ni kutaka kuzungumzia ukomo wa jumla wa nguvu za kufanya kazi, hii haijalishi aina ya kazi uliyonayo.
Uchunguzi uliofanywa na watafiti wengi duniani kuhusiana na madhara wanayokutana nayo wastaafu wa kazi za kuajiriwa sambamba na wale wanaokumbwa na umri mkubwa wa kushindwa kumudu kufanya kazi umebaini kuwa, watu wengi wamekosa elimu ya kuwawezesha kujua ni wakati gani wa kujiandaa ili kuingia katika tenga hilo la maisha yanayomnyima mhusika fursa ya kujitumikia kwa nguvu zake.
Wengi kati ya wazee waliochunguzwa ambao maisha yao yalionekana ni ya shida na kukatisha tamaa, tangu wale waliokuwa na kazi za kujiajiri mpaka wale waliokuwa wameajiriwa katika viwanda na sekta  mbalimbali waligundulika kuwa katika maisha yao ya ujana, kustaafu na kufikiria uzee haikuwa sehemu ya mawazo yao, badala yake waliishi kwa kudhani hali walizokuwa nazo zingedumu, hivyo hawakuwa na hofu ya kuja kuishiwa nguvu na kustaafu kazi.
Hata hivyo, ukweli wanaokubaliana nao watafiti hao wa masuala ya kazi na maandalizi ya uzeeni  ni kuwa, mipango ya kustaafu lazima ianze tangu siku ya kwanza mhusika anapoajiriwa kama mfanyakazi au pale anapoingia katika harakati za kimaisha kwa kujitafutia riziki. Wanasema mawazo ya kufikiria uzee na siku za kushindwa kufanya kazi ndiyo yanayochochea juhudi za kimaendeleo, uwajibikaji na utunzaji wa akiba za baadaye.
Hivyo basi, mtu anayetaka kuishi vema baada ya kufikia ukomo wa kufanya kazi ni lazima asiuone ujana kuwa si sehemu muhimu ya kustaafu, wala asidhani uzee unawahusu wenye umri mkubwa, bali auchukulie uwezo wake wa kufanya kazi kama jibu la maisha yake yajayo.
Kustaafu si kitu kinachotokea kwa kushtukiza, bali huja taratibu. Jambo la msingi ni kuzingatia mambo 3 yafuatayo ili uweze kuepuka tabu za maisha baada ya kustaafu au kukosa uwezo wa kufanya kazi. Lakini kubwa zaidi unaloweza kunufaika nalo kwa kuzingatia haya ni kujipatia maendeleo.

KUJIANDAA KIAKILI
Watu wengi hasa wenye kazi za kuajiriwa huwa hawafikirii kuwa kuna siku watakuja kuishi bila kazi. Hawawazi juu ya kufikia ukomo wa nguvu za kumudu majukumu yao ya kazi. Hawaziandai akili zao, ili ziwe tayari kukubaliana na maisha ya uzeeni, ukosefu wa kazi na hata siku za kuugua magonjwa yasiyoponyeka haraka. Ndiyo maana utawakuta watu wanaponda maisha na kutapanya mali kwa kuamini kuwa kesho ya kupata mshahara ipo, huku wakiisahau kesho kutwa ya kukosa mshahara, kustaafu na kukosa nguvu za kufanya kazi.
Kosa hili la kutokujiandaa kiakili ndilo linalochangia wastaafu wengi kupoteza maisha yao muda mfupi baada ya kukosa kazi. Hii inatokana na msongo wa mawazo unaokuja akilini mwao ukitaka kutafuta majibu ya namna ya kuishi katika maisha mapya, ambayo hawakuwahi kuyawaza kabla. Jambo hili ni la hatari sana na wala haipendezi mtu awaze namna ya kuishi baada ya kuwa ameacha kazi au amekosa uwezo wa kujishughulisha.

 KUCHAGUA SEHEMU YA KUISHI
Jambo la pili ambalo ni kubwa ni mtu kuchagua mapema sehemu atakayoishi pindi atakapofikia umri wa kustaafu. Watu wengi waliopo makazini au walio na nguvu za kufanya kazi hawachagui sehemu watakayoishi pindi watakapofikia ukomo wa kufanya kazi. Ndiyo maana hawana majibu sahihi ya wapi wanatarajia kuhitimishia maisha yao.
Utamkuta mtu anafikia umri wa kustaafu hajajenga walau banda la kuweka ubavu! Eti wakati anapokabidhiwa malipo yake ndiyo anachukua jukumu la kununua kiwanja na kutaka kujenga nyumba, kitu ambacho huwa kigumu na wengi wamekwama.
Jambo la kuzingatia hapa ni kuwa wakati ukiwa na nguvu weka misingi ya wapi utaishi, kama ni mjini au kijijini ulikozaliwa. Baada ya uamuzi huo fanya kila uwezalo kuyazoea mazingira na jamii inayoishi kule ulikopanga kuishi. Jenga huko walau kakibanda kadogo. Usingoje kujenga utakapopata fedha za mafao.

Comments